Wednesday, November 13, 2024

Miaka 7 iliyopita, kipindi nikiwa chuo, nilibeba ujauzito wa huyu mwanaume. Baada ya kumwambia Mama yangu, aliniambia nitoe mimba bila kumwambia mwanaume kuwa nina mimba yake.


Miaka 7 iliyopita, kipindi nikiwa chuo, nilibeba ujauzito wa huyu mwanaume. Baada ya kumwambia Mama yangu, aliniambia nitoe mimba bila kumwambia mwanaume kuwa nina mimba yake.

Ni kwa sababu mwanaume alikuwa ni bodaboda tu, hivyo mama alimkataa. Aliniambia nisimwaambie mtu yeyote, kipindi hicho ndiyo nilikuwa naelekea kumaliza chuo, hivyo niliamua kuachana na mwanaume na kubadilisha mawasiliano na kila kitu.

Nilitaka kutoa ile mimba, lakini ilinisumbua sana na hatimaye nikajifungua mtoto ambaye sasa ana miaka 6. Ni mkubwa na amefanana na baba yake kila kitu. Baada ya kumaliza chuo, nilihangaika kutafuta kazi lakini mpaka leo sijafanikiwa, hivyo niko sehemu ambapo najitolea na pia nina biashara ndogo.

Wiki mbili zilizopita nilimuona yule mwanaume mtandaoni. Alioa na ilikuwa harusi kubwa alipostiwa na MC mmoja hivi. Nilipoangalia vizuri, niligundua kuwa sasa ni mfanyabiashara mkubwa tu na ana duka la spea ambalo analitangaza mara kwa mara.

Nilifuatilia mpaka nikafika dukani kwake, lakini sikumkuta; nilikuta wafanyakazi wake tu. Kusema kweli niliumia kwa sababu huko nyuma mwanaume alinipenda sana, hata nilipomwacha alinisumbua sana, lakini kwa sababu ya mama, nilimuacha.

Natamani kumtafuta mwanaume na kumwambia kuwa aliniacha na mimba yake, nina mtoto wake na najua akimuona atamkubali. Nataka mtoto wangu aishi maisha ya hadhi yake, yaani afaidi matunda ya baba yake.

Najua nilikosea kumficha lakini nahisi kuwa mtoto ana haki ya kumjua baba yake. Je, nitakuwa nimefanya kitu kibaya kumtafuta mwanaume? Naomba ushauri wako!

No comments:

Post a Comment