Wednesday, November 13, 2024

π——π—˜π—”π—₯ 𝗠𝗔𝗠𝗔


🚨_|| π——π—˜π—”π—₯ 𝗠𝗔𝗠𝗔 ♥️πŸ₯Ί

➡️ Mwambie anipigie ni mimi mama yake!!

➡️ Mwambie sina simu ila nimeona picha zake kwenye simu ya kupalaza ya khamisi.Mwambie amenenepa sana 

➡️ Mwambie nimeona gari lake ni zuri sana !!ila mwambie mama yake bado naishi kwenye lile banda pamoja na kuku.

➡️ Mwambie nimeumwa sana ila nikapona bila hata kutumia dawa.

➡️ Mwambie mzee juma bado ananidai pesa zake nilizokopa ili nimlipie ada amechukua kile kishamba nilichokuwa nakitegemea kufidia deni lake.

➡️ Mwambie mimi mama yake nimebaki pekee yangu tangu baba yake kafariki sina hata wa kunisogezea kuni motoni.

➡️ Mwambie leo nimetamani sana nyama😭 zile mboga zilizoota zenyewe upenuni zimenichosha mpka mdomo umekuwa mchungu.

➡️ Mwambie wale vijana walitaka wanipige eti mimi mchawi.

➡️ Mwambie mama yake nimekuwa mzee sana nahesabu siku tu aje hata nishike mikono yake nimuoneshe mipaka ya nyumba yetu/!!

➡️ Salio limeisha mwambie mama anampenda sana😭!ila huku kijijini nimebaki pekee yangu wenzangu wote wameenda mjini kusherekea kwa watoto wao...

😒😒 TUSIWASAHAU WAZAZI WAKUU πŸ˜­πŸ’”πŸ™πŸΎ

No comments:

Post a Comment